Tuesday, March 8, 2011

Wa Chini, Mkia na kucha zake......

Duma (au wa chini kama alivyozoeleka kwa wazee wa Pori) ni mnyama ambae anasifika kwa uwezo wake wa kutimua mbio haraka na kuwashinda wapinzani wake. Maandiko ya kitaalam yamewahi andika kuwa wa chini ana uwezo wa kufikia kasi ya Km 112 kwa saa. akiwa ktk kasi hii, wa chini anaweza kwenda umbali wa mita 7 hewani bila ya kugusa chini.

Unapokuwa na uwezo mkubwa wa spidi kama alio nao wa chini, ni lazima uwe na uwezo mzuri wa ku-balance mwili wako unapokuwa unakimbia full spidi. ktk hili, wa chini anatumia vitu viwili ambavyo mwenyezi Mungu amemjalia - Mkia na kucha zake. Anapokuwa anakimbia full speed, wa chini huutumia mkia wake kupata balance anapokata kona kali ili kwenda sambamba na kile anachokikimbiza. Mkia wake ni hazina kubwa sana inayomwezesha kushinda wapinzani wake ktk mbio fupi. Mara nyingi wa chini anapokuwa anakimbia, huuinua mkia wake juu ktk hali inayompa balance nzuri ya mwili wake ktk spidi kali.

Ili kumhakikishia kuwa anaweza kuchanganya mwendo haraka, wa chini amejaliwa kuwa na kucha ambazo huwa zinakuwa nje kwa kiasi kikubwa tofauti na 'paka' wengine ambao kucha zao hufichwa ndani ya miguu yao ha hutolewa nje wakati wa mapambano au kula. wenye lugha yao wanasema kucha za wa chini ni semi retractable. kucha kuwa ktk hali hii kunamsaidia wa chini kama vile tairi ya gari yenye kashata nzuri inavyoweza kumsaidia dereva katika mazingira ya tope au mchanga. (picha | Ngorongoro, TTB)

1 comment:

  1. kwa nyongeza cheeter pia husaidiwa na mwili wake kuwa slender na udogo wa kichwa. wataalamu humwita Acinonius jubantus. Inaaminika kuwa speed yake inaweza kuongezeka mpaka 120. ikumbukwe kuwa ni Day active(Diunal)kwa maana hufanya kazi zake mchana zaidi na usiku hupumuzika hufanya hivyo kukwepa maadui zake wafanyao kazi usiku kama vile simba,chui na fisi. Kwa kifupi hawapendi competition kwani wana uwezo wa kuchase mnyama na kwa sababu hiyo huonewa sana na maadui zake na ndio maana hawapendi matatizo na ni wapole sana. Moses.

    ReplyDelete