Monday, March 14, 2011

Hapa napo ni Tanzania pia....

Anony wa March 18,2011 0635PM ametoa jibu Sahihi
Picha hii imepigwa eneo lijulikanalo kama view point lililopo hifadhi ya taifa ya manyara. barabara mnayoiona ni barabara inayotoka mtu wa mbu kuelekea Karatu, Ngorongoro, Serengeti na kwengineko. Kibanda chenye paa jekundu ni sehemu ambapo kuna parking ya magari kwa wale wanaopenda kuiangalia hifadhi ya Manyara tokea juu, upande wa pili wa barabara na hapa kilipo kibanda. kibanda chenyewe ni maliwato. Hii ni moja ya sehemu unazoweza kuliona bonde la ufa vyema, kingo zinazoonekana ni za bonde la Ufa. Picha hii niliipiga nikiwa nimesimama pembezoni mwa bwawa la kuogelea lililopo ktk hotel ya lake Manyara Serena lodge. Shukran kwa wengine mliojaribu kubashiri.

6 comments:

 1. kaka wapi hapa?

  ReplyDelete
 2. maridadi kweli, inabidi kujenga lodge hapo kulia, view yake si mchezo

  ReplyDelete
 3. Naungana na wapendao kujua ni wapi hapa!

  ReplyDelete
 4. simon, japo mhusika amechelewa kusema ni wapi hapo, jamaa yangu mwenye jicho la tai kasema hapo ni Manyara - kibanda pale mbele ni msalani.

  ReplyDelete
 5. Juu ya milima ya lukumbule kama unaenda songea

  ReplyDelete