Friday, February 11, 2011

Itakuwa ni weekend ndefu ki ukweli.... April 2011

Weekend hii inaanzia tarehe 22-04-2011 (Ijumaa kuu) na kuishia 26-04-2011 (Muungano). Kwa kifupi, ukiondoka kazini Alhamisi, unarudi kazini Jtano wiki ijayo. Ni nafasi murua kwa wale wanaopenda kupotea mjini na kwenda mbali kupumzisha mwili na akili. Ni fursa nzuri pia kwa mdau unayependa mambo ya porini lakini muda umekuwa kikwazo kwako. Anza sasa kudodosa na kuweka mkakati.

Kwa makampuni yanayoandaa safari za kwenda kwenye hifadhi mbalimbali, karibuni kunadi safari zenu ktk blog yenu ya utalii. - TembeaTz. Tumeni matangazo yenu kupitia tembeatz@gmail.com nasi tutayaweka hewani. Tunapendelea zaidi zile safari zinazowalenga wazalendo.
Unaweza pia kushiriki ktk kura ya maoni iliyopo upande wa kulia kwako wa blog hii.

1 comment:

  1. Duh! Ahsante kwa kunihabarisha, naanda mazingira ya kupotea

    ReplyDelete