Tuesday, December 14, 2010

Tumbusi - Tarangire NP

Awali tulidhania mkusanyiko wa Tumbusi hawa ulihusiana na mnyama aliyekufa, lakini tuliposogea karibu tuligundua ya kwamba walikuwa wameshuka kuja kunywa maji na kumpumzika.

Uwepo wa Tumbusi wengi huweza kuashiria windo na ktk hali ya kawaida, mwindaji anaweza akawa karibu ya kundi la Tumbusi. Lakini kuna nyakati, ndege hawa huja ardhini kupata mahitaji mengine ikiwemo kupumzika. Muda mwingi huutumia kuruka juu angani ktk aina ya mruko ijulikanayo kama Thermal Soaring. Style hii hutumia na mwewe pia. Inawawezesha ndege hawa kukaa angani kwa muda mrefu bila ya kutumia nguvu nyingi kipiga mbawa zao. Shida moja ya aina hii ya Mruko ni lazima hewa iwe imepata joto kidogo ndio iwe na uwezo wa kumsaidi ndege kufanya thermal Soaring.

Picha zote zimepigwa Hifadhi ya Taifa ya Tarangire, pembezoni mwa mwto tarangire, karibu na Matete picnic site

No comments:

Post a Comment