Tuesday, December 21, 2010

Njia mbadala ya kuwalinda Faru wetu (PJ)

Kifo cha Kifaru George (12) kilichotekea hivi Karibuni huko Serengeti kimevuta hisia za wengi katika namna tofauti. Wapo walioanza kwa kutoa namna za kuongeza ulinzi kwa wanyama hawa adimu na wapo ambao wameamka kwa kuinyooshea kidole Serikali na taasisi zake zenye dhamana ya kulinda na kuwahifadhi wanyama hawa dhidi ya majangili. Inaelezwa ya kwamba Faru huyo ameuwawa na majangili ambao baada ya kumuua, walitokomea na pembe yake. Ukweli wa mambo ni kwamba majangili hao walikuwa na nia ya pembe ya faru huyo na si kitu kingine.

Katika kundi la watu walioanza kufikiria namna ya kuwalinda wanyama hawa (na wengineo), nimefurahishwa na comments alizotoa Paul James wa Clouds FM ktk kipindi cha power breakfast leo asubuhi.
PJ (kama anavyojulikana na wengi) alisema kwa kuwa Pembe za Faru zinatumika (mashariki ya mbali na Asia) kuwasaidia watu wenye matatizo ya 'Jogoo kushindwa kupanda mtungi', kwanini nchi hizo wasipewe namna mbadala ya kushughulikia tatizo hilo kwa kutumia miti shamba ambayo ipo kwa wingi hapa nchini na kwengineko? PJ alienda mbele kwa kutaja jina la Mkuyati, mti/dawa ambayo inaelezwa ya kwamba inawasaidia watu wenye shida hizo na kuleta hali ya bendera chuma, mlingoti chuma..
japo comments zake zimekaa kimzaha mzaha, lakini ni jambo ambalo linaweza kuangaliwa ili kutokomoze mauaji haya. Swala hili linahitaji kuunganisha nguvu za pamoja baina ya wahifadhi wa wanyama pori, wataalam wa misitu, wataalamu wa afya(hususan maswala ya Jogoo kushindwa kupanda mtungi) ili kuweza kupata suluhu. Si vibaya kuliangalia hili kwa mtizamo huu
Picha zote mbili zilipigwa na timu ya tembeaTz ndani ya Ngorongoro crater. Faru anayeonekana sio Faru George aliyeuwawa huko Serengeti.

No comments:

Post a Comment