Friday, December 10, 2010

Mandhari ya Ngurdoto Museum

Ngurdoto Museum ipo ndani ya hifadhi ya taifa ya Arusha. Ni eneo ambako kuna jengo dogo linaloelezea historia ya hifadhi hii. Unaweza jikumbusha habari za makumbusho hii kwa kubofya hapa. Mtundiko huu unakuonyesha sehemu ya nje ya Makumbusho hii

Ingekuwa mjini hapa kungejengwa kipita shoto (keep-left) lakini porini hata triangle inawezekana. Ukinyoosha mbele unakuwa unaelekea ilipo Ngurdoto crater ambayo nayo ipo ndani ya hifadhi ya taifa ya Arusha. Njia inayoelekea Kushoto inaelekea upande mwingine wa hifadhi ambako huko unakutana na Maziwa ya Momella - Momella kubwa na Momella Ndogo. picha toka maktaba ya Tembeatz

No comments:

Post a Comment