Ni makumbusho ambayo ipo ndani ya hifadhi ya taifa ya tarangire. Kibanda unachokiona ktk picha ya juu ndio makumbusho yenyewe.
Makumbusho ya ngurdoto inavyoonekana kwa mbele. Barabara inayoendelea mbele ndio inayoelekea ilipo Ngurdoto crater. Ukichepuka kushoto hapo utakuwa unaelekea yalipo Maziwa ya Momella na geti la Momella.
pia makumbusho hii ina taarifa mbalimbali zinazoihusu hifadhi hii. Ilivyoanzisha na mpaka ilipo sasa. Ni sehemu nzuri ya kusimama na kupata dondoo mbalimbali zinazoihusu hifadhi ya Arusha. Kuna mafuvu kadhaa ya wanyama yamehifadhiwa ndani ya makumbusho hii. Unaweza simama hapa kwa lengo la kutembelea makumbusho au (na pia) kuchimba dawa. Kuna vyumba vya adam na hawa maeneo haya
No comments:
Post a Comment