Thursday, December 23, 2010

Dinner at the lagoon, Ras Kutani

Mchana, sehemu hii hutumika kama bandari ya kupokelea wageni wanaofika Ras Kutani kwa ndege na kuletwa hadi hotelini kwa boti. Jua likizama, sehemu hii hugeuka sehemu ambayo wageni wanaokuwa hapo hotelini wanaweza andaliwa meza na kupata chakula cha usiku hapo. Mgeni anayepewa huduma hii ni yule ambae yupo fungate (na akaujulisha uongozi kuwa yupo fungate) au mgeni yeyote atakae penda kupata dinner yake mahali hapo na kuwasilisha ombi lake kwa uongozi wa Hoteli. Picha juu ni sehemu hiyo ikiwa ktk hatua za awali za maandalizi kwa jioni hiyo.

Inapendeza kwa wawili lakin hata wanne panafaa pia.

Maandalizi yakiwa yanaendelea

Mlima wa mchanga unaotenganisha bahari ya Hindi na lagoon

Lagoon ikionekana na sehemu ya msitu wa kufanyia Lagoon walk unavyoonekana kwa mbali.

1 comment:

  1. Hii lagoon ipo mkoa gani? Panaonekana ni pazuri sana.

    ReplyDelete