Monday, November 15, 2010

Epuka Ajali uwapo porini

Kama kuna sehemu ambayo dereva anahitaji kuwa makini zaidi ni pale anapokuwa anaendesha gari ndani ya eneo la hifadhi tena hifadhi yenye wanyama wakali. Gari analotumia wakati huo sio tu ni chombo cha usafiri bali kwa namna moja au nyingine ni chombo kinachomhakikishia usalama wake na abiria alionao. Ili kuongeza umakini, dereva atakayesababisha ajali ndani ya eneo la hifadhi hupigwa faini ambayo inaweza kufika hadi TSH 200,000 hata kama ajali hiyo haikuhusisha mnyama. Hali huwa mbaya zaidi kwa dereva endapo ajali hiyo itakuwa imehusisha mnyama na mnyama huyo akawa ameumia au kupoteza maisha. Zingatia hili hata kwako mdau ambae utakuwa unakatisha hifadhi ya mikumi uwapo safari. Spidi ndani ya hifadhi haipaswi kuzidi km 50 kwa saa. Shukran ya picha kwa mdau JSK wa moshi aliyetembelea Ngorongoro crater hivi karibuni

No comments:

Post a Comment