Thursday, October 14, 2010

Wapo Harusini, Selous

Mdau Tom aliwakuta hawa sharubu wawili wakiwa harusini pembezoni mwa ziwa la Nzerekela ndani ya pori la akiba la Selous.


Hii ndio harusi yenyewe. Sharubu hutumia muda wa siku takriban nne katika shughuli hizi lengo likiwa ni kuendeleza kizazi na jamii yao.

Mapumziko ya hapa na pale huwa yanakuwepo.

Mara nyingi sharubu wanapokuwa harusini au honeymoon huwa wanakaa eneo moja kwa kipindi kirefu. hali ambayo hutoa nafasi kwa wageni wanaopenda kuona sharubu kuwapata kirahisi. Dereva anapopata taarifa kuwa kuna sharubu wapo harusini mahali fulani, huwa anajau hana haja ya kuharakisha kwani hao atawakuta tu hata kama ni baadae. ahsante ya picha kwa mdau Tom wa Kima Safaris

2 comments:

 1. Siku nikienda kuwaona nitawapa taarifa kuwa mliwachungulia wakati wa hanemuni yao na kuwapiga picha, we ngoja tu.
  teh teh teh
  Asante Tom
  Asante KK

  ReplyDelete
 2. Na kweli subi, amewapiga chabo!!!

  ReplyDelete