Monday, September 13, 2010

Singita Sasakwa lodge, Grumeti reserve

Singita Sasakwa Lodge ni moja ya hotel tatu zinazomilikiwa na kampuni ya Singita Game reserves. Hotel hizi zote zimejengwa ndani ya pori tengwa la Grumeti, pori ambalo linasimamiwa na kuendeshwa na kampuni ya Singita. Picha juu ni sehemu ya moja ya chumba cha wageni ktk lodge hii.

Baadhi ya vyumba vinakuwa na sebule kwa ajili ya wageni kupumzikia na kuota moto kipindi cha baridi kali huko ndani ya pori la Grumeti

Mlango mkuu wa kuingilia Sasakwa lodge

Hii ni moja ya vyumba ambavyo vinakuwa na bwawa la kuogelea linalojitegemea (kwa ajili ya yule aliyefikia chumba hicho tu). Sambamba na hilo, chumba kina veranda ambayo inampa mgeni muonekano mzuri wa mandhari ya pori la Grumeti na hifadhi ya taifa ya Serengeti pia.

Unapata Dinner kwenye Veranda huku ukifurahia mandhari mwanana ya Grumeti reserve na hifadhi ya taifa ya Serengeti kwa mbali. Unaweza kupata dondoo zaidi kuhusu Sasakwa Logde kwa kubofya hapa [picha - Natalie, Singita game reserves]

No comments:

Post a Comment