Monday, September 13, 2010

Ngorongoro Crater

Crater ya Ngorongoro inavyoonekana toka Crater view point. Unapokuwa hapa kipindi baada ya mvua, unaweza ukasema kwamba crater ni kama bwawa kwani sehemu kubwa huonekana ni kama imejaa maji. La hasha, hilo ni moja ya maajabu ya ngorongoro crater, unatakapoingia ndani unaweza usiona maji mengi kama ulivyodhania. Hii hali huwachanganya wengi ambao hutembelea ngorongoro wakati wa mvua au baada ya mvua kunyesha. Unaweza gairi safari yako kwa kuhofia matope au madimbwi. Ndani ya crater mambo yanakuwa mswano...

Hapa ni kwenye geti la kuingilia crater (crater descend). Wageni wote wanaingia crater huingilia hapa. ukiwa hapo unapata view mwanana ya mandahari ya crater na ziwa Magadi pia. Barabara uionayo pembezoni mwa huo mteremko, chini kwenye crater ndio barabara uiayotoka kwenye geti la kuingilia na kuendelea ndani ya crater. Wageni hutokea sehemu tofauti na walipoingilia. Taswira hizi zilipigwa mapema mwaka huu na Mdau Bonny wa Karibu Fair Arusha Siku hii kulikuwa na manyunyu ya mvua yaliyoleta ukungu kiasi kwa maeneo ya juu. Crater kwenyewe mambo yalikuwa poa na wanyama walionekana kama kawa.

No comments:

Post a Comment