Monday, September 13, 2010

Hot Air Balloon zaanza safari Tarangire NP

Baada ya kukabidhiwa leseni ya kuendesha shughuli za safari za Hot Air Balloon ndani ya hifadhi ya Tarangire mapema mwaka huu, Kampuni ya Adventures Aloft (T) ltd ilianza rasmi safari zake mnamo tarehe 25 Julai 2010. Mpaka sasa kampuni hii ina pulizo moja kubwa lenye uwezo wa kubeba abiria 16 kwa safari moja. Safari zao huanzia eneo lijulikanalo kama Boundary hill gate na huchukua takriban saa moja na ambapo huwa linakuwa limesafiri umbali wa takriban kilomita 15

Mgeni hupata fursa ya kujionea mandhari ya hifadhi ya taifa ya Tarangire na maeneo jirani akiwa juu kwenye hot air balloon. Mto Tarangire unakuwa unaonekana kama ilivyo ktk taswira ya juu na nyingine hapa chini. Ni mto ambao unapita ktk hifadhi ya Tarangire.

Hapa rubani alikuwa amelipandisha balloon juu zaidi

Safari huanza saa kumi na mbili na nusu asubuhi ambapo mpango ni ule ule wa mgeni kufuatwa toka alipofikia na kuletwa eneo la kurukia ili kuanza safari yake kama ilivyo pangwa. Baada ya safari ya Balloon abiria hupata fursa ya kupata kifungua kinywa cha pamoja ktk eneo litakaloteuliwa ndani ya hifadhi. Baada ya kifungua kinywa mgeni anakuwa huru kuendelea na ratiba yake binafsi.
Wasiliana na kampuni yoyote inayoshughulika na kupeleka wageni porini upatiwe mpango mzima wa kufanya safari ya hot air balloon huko Tarangire NP. Shukran zimfikie Nd Uruka, Park Warden - Tourism kwa taswira zote za mtundiko huu na pia Capt Andrew kwa maelezo ya zaida khs safari hizi.

No comments:

Post a Comment