Tuesday, September 14, 2010

Gharama wanayoingia "wao" kuja kwetu

Mara kadhaa baadhi ya makampuni na wadau mbalimbali ktk sekta ya utalii wamekuwa wakiandaa safari za makundi kwa ajili ya wazalendo kwenda kutembelea hifadhi za hapa nyumbani. zipo safari ambazo zilifanikiwa na zipo ambazo hazikuweza kufanikiwa. Ktk moja ya mchakato wa kura ya maoni iliyopata kuendeshwa na blog hii, kipengele cha gharama kiliibuka kidedea kama moja ya vitu vinavyowazuia wazalendo kutembelea hifadhi zetu.
Leo naomba mniruhusu niwaonyeshe upande wa pili wa shilingi ili tuweze kupata picha ni namna gani wenzetu wanavyogharamika kuja kutembelea nchi yetu na vivutio vyake.
ktk pitapita zangu kwenye mtandao nilikumbana na moja ya tovuti ambayo ilikuwa na safari iliyotangazwa huko majuu mahususi kwa ajili ya familia ambazo zingependa kuja kutembelea vivutio vilivyopo hapa nyumbani

Mpango wao ulikuwa kama hivi,
$6,690 adults and teens 16-18;
$6,354 children 12-15;
$5,054 children 8-11.
Prices are per person, based on double occupancy. Single supplement: $990.
Bofya hapa upate kujua zaidi

No comments:

Post a Comment