Thursday, September 2, 2010

Geti la Tarangire

Katika hifadhi nyingi hapa nyumbani, palipo na geti la kuingia ndani ya hifadhi au pori la akiba huwa kunakuwa na vitu mbalimbali ambavyo wengi wetu huwa hatuvioni kutokana na shauku ya kuingia ndani ya hifadhi. Hifadhi nyingi zimekuwa na sehemu za kutoa taarifa mbalimbali kuhusu hifadhi, mazingira ya hifadhi na wanyama wanaopatikana ktk hifadhi husika. Ktk geti la kuingilia ndani ya hifadhi ya taifa ya Tarangire hali ipo hivyo pia. Kuna kituo cha taarifa kwa wageni, na vitu mbalimbali vinavyoelezea maisha ya wanyama. Ktk baadhi ya hifadhi (hususan zile zenye mageri mengi vituo hivi hujengwa katikati ya hifadhi. Mfano wa hii ni hifadhi ya taifa ya Serengeti ambappo kituo cha taarifa mbalimbali kuhusu Serengeti kipo maeneo Seronera, ndani ya hifadhi.

Njia hii inakupeleka sehemu yakufanyia malipo ya huduma mbalimbali ikiwemo viingilio vya kuingilia ktk eneo la hifadhi

Adam na Hawa

Kibanda unachikiona ni kibanda cha walinzi, hiyo land rover unayoiona ndio inaingia hifadhini rasmi. licha ya kwamba hapo niliposimama mimi wakati nikipiga picha ni eneo la hifadhi pia. Kwani usiku hapo wanyama wanakuja na kupiga misele yao.

No comments:

Post a Comment