Friday, August 13, 2010

Taswira maridhawa - Arusha NP

Mara kadhaa nilizowahi tembelea hifadhi ya Taifa ya Arusha nimekuwa nikifanya safari ambayo huwa inachukua sura inayofanana na mwelekeo wa mshale wa saa (clockwise direction). Hivi Karibuni nilibadili utaratibu na kuanzia upande tofauti na nilivyozoea. Ndipo nilipobaini muonekano mzuri wa nyumba hii ambayo ipo ndani ya hifadhi ya Arusha, katika moja ya Misitu iliyopo ktk hifadhi.

Ni Nyumba iliyojengwa kwa mbao ktk eneo lenye nyasi mwanana na kuipa mandhari nzuri.


Nyumba hii inatumiwa na watafiti toka ktk chuo cha usimamizi wa wanyamapori cha Mweka (College of Africa Wildlife Management-CAWM). Watafiti hukaa ktk nyumba hii pindi wanapokuwa wanafanya tafiti mbalimbali za wanyama na mazingira yao ktk hifadhi ya taifa ya Arusha.


No comments:

Post a Comment