Hii ni barabara toka njia panda Makuyuni kuelekea Ngorongoro, Manyara, Serengeti hadi mkoani Mara. Ni Moja ya barabara muhimu sana kwa sekta ya utalii kwa kanda ya Kaskazini ya Utalii. Makuyuni ipo ktk njia itokayo Arusha kuelekea Babati mpaka Dodoma. Ukikata kulia hapo utakuwa unaelekea Ngorongoro, Serengeti na kwengineko. ilhali ukinyoosha mbele (Linapotokea gari) utakuwa unaelekea Babati hadi Dodoma pia. Njia hiyo pia (ukinyoosha) itakufikia kijiji cha Kwa Kuchinja ambapo utakutana na njia panda ya kuelekea geti la hifadhi ya Tarangire.
Huu ni 'Mkeka' ambao unaanzia makuyuni (baada ya kukata kulia) ambao ndio utakaokupeleka Ngorongoro, Manyara, Serengeti na mpaka mkoani Mara na hata Mwanza. Japo 'mkeka' unaishia ktk geti la kuingilia ktk hifadhi ya Ngorongoro.
Baada ya kupita njia panda ya Makuyuni, utaanza kuliona Ziwa Manyara japo kwa mbali lakini si haba, linaonekana. ktk taswira ya juu, Ziwa Manyara linaonekana kama kitu cheupe chini ya hiyo milima. Kwa kifupi, barabara hii ipo ndani ya bonde la ufa na milima uionayo kwa mbali ni kingo za bonde la ufa
Ukiwa ktk baadhi ya sehemu ambazo barabara imenyanyuka kidogo, unakuwa unapata mandhari maridhawa ya Ziwa Manyara na baadhi ya maeneo wanamoishi jamii za Wamaasai.
No comments:
Post a Comment