Monday, August 23, 2010

Geti la Ngongongare - Arusha NP

Katika mageti mengi ya hifadhi za taifa na mapori ya akiba, huwa kunakuwa na maelezo kuhusu eneo husika. Geti la Ngongongare nako pia kuna hiyo hali. Mabango uyaonayo yana maelezo kadha wa kadha kuhusu hifadhi hii. hali humsaidia mgeni kujua mambo mengi zaidi kuhusu hifadhi husika ukiachia mbali wanyama wanaoishi huko.

Kibanda ukionacho ndicho ambacho walinzi 'wahifadhi' hukaa kujikinga na jua wakati wa mchana kwa lengo la kukagua vibali vya wageni wanaoingia ktk hifadhi ya Arusha

2 comments:

  1. Vibali vya wageni wanaoingia ktk hifadhi ya Arusha vinapatikana wapi?
    Mdau Uholanzi

    ReplyDelete
  2. Mdau Uholanzi,
    Vibali vinapatikana hapo hapo ktk geti la Ngongongare, kwa yule atakaeingia kupitia geti hilo.
    Huna haja ya kufanya booking mapema wala nini, wewe andaa mkwanja wako.
    kwa Mtanzania kiingilio ni TSh 1,500 (mtu mzima) na gari 4WD(10,000). Kibali ni cha masaa 24.

    Natumai nimejibu swali lako, kama lipo hujafahamu usiste kuuliza. Ukipenda tuma email kupitia tembeatz@gmail.com kwa maelezo zaidi ya kina.

    Ahsante,
    tembeatz.blogspot.com

    ReplyDelete