Tuesday, May 4, 2010

Kiota cha Fundi Chuma

ktk mapori na hifadhi za hapa nchini na kwengineko africa, ndege ajulikanae kama fundi chuma hupatikani (kwa bahati mbaya maktaba ya TembeaTz inasaka taswira yake). Ndege huyu ni maarufu kwa kujenga viota vikubwa na imara sana. Ujenzi hufanywa na dume kwa lengo la kumrubuni jike ili aungane nae kuanzisha familia kama ilivyo ada kwa ndege wengi.
Fundi chuma hujenga viota vikubwa na kwa kutumia malighafi mbalimbali ambazo anaweza kuzipata ktk maeneo anayopita. hutumia udongo, miti, mawe madogo madogo na wakati mwingine hata vipande vya mifuko ya plastiki na nylon vimewahi kutwa ktk kiota cha fundi chuma. Ilihali ndege wengine hutumia miti na majani kutengenezea viota vyao.

Jambo moja ambalo lilipita masikioni mwangu ni kwamba, cheza mbali na kiota cha fundi chuma. Inaelezwa ya kwamba (sina ushahidi) ukikiharibu au kubomoa kiota cha fundi chuma (ndege), basi kama ulikuwa una nyumba yako, hiyo nyumba yako ipo hatarani kupotea kwa namna yoyote ile - mafuriko au moto. wapashaji habari walienda mbele na kusema kuwa endapo kama hauna nyumba, basi nafasi ya wewe kuja kuwa na nyumba yako ndio inakuwa imetoweka.

Nilidokezwa ya kwamba hii dhana ipo miongoni mwa makabila mengi ya hapa nchini. Ukweli ni kwamba hii issue ni kama sumu, haionjwi! so ukweli wake inabidi uupate kwa kupitia neno la mdomoni. Mara nyingi fundi chuma huwa na tabia ya kukikacha kiota chake endapo atagundua kuwa hakivutii majike.

picha juu ni kiota cha fundi chuma (hilo fungu unaloliona ktk huo mti) kilichojengwa ktk mti pembezoni mwa Mto Ruaha, ndani ya Ruaha NP. Ahsante ya picha kwa mdau Thom wa Kimasafaris.

1 comment: