Saturday, April 17, 2010

wapo wanaolitafuta joto

Wakati bwana afya anakuwa anahaha kulikimbia joto ambalo linazalishwa mwilini mwake wakati wa mmeng'enyo wa chakula, wapo wanyama ambao ili waweza kuishi vizuri ni lazima waipashe joto miili yao. Mkasi (Mamba) ni mmoja wa wanyama ambao wapo ktk kundi la wanyama wenye damu baridi.
Mkasi hutegemea zaidi joto la mazingira ili kuweza kumsaidia kupandisha hali ya joto la mwili wake kufikia kiwango kinachomwezesha kufanya shughuli zake za kila siku. Asipoweza kufanya hivyo, mkasi hushindwa kuwinda kitu chochote. picha juu ni mamba akiota kijua cha asubuhi ktk 'kisiwa' kilichokuwa ndani ya mto Rufiji, nje kidogo ya pori la akiba la Selous.

No comments:

Post a Comment