Monday, April 12, 2010

Sababu za ugomvi wao zinaeleweka

Ugomvi baina ya wanyama hususan wanyama wa jamii moja huweza kusababishwa na moja ya sababu zifuatazo; Malisho, Eneo (territory) au uzazi (kugombani mwenza). Hizi ndizo sababu kuu 3 ambazo zinaweza pelekea wanyama wa jamii moja kushindwa kuelewana kiasi cha kuamua kutunishana misuli kwa nia ya kupata suluhu baina yao.

Kwa viboko, ugomvi wao hauishi mpaka mmoja akubali kushindwa. Hii hufikiwa muafaka kwa aliyeshindwa kulala chini na kisha mshindi kumpanda kwa juu. Kwa viboko, wanoongoza kwa kupambana wenyewe kwa wenyewe ni madume, kwani ndio wanaomiliki eneo ktk bwawa na majike waliomo humo. Majike wao huingia ulingoni kulinda watoto tu na hapo atakae kuwa anashambuliwa huwa ni mnyama wa jamii nyingine.

Wakati mpambano huo ukiendelea nje ya bwawa, viboko wengine (majike na Juveniles) wamebaki ndani ya bwawa wakisubiri kipenga kitakachoamuru mshindi ni nani. Endeapo mtawala wa hapo atashindwa ktk mpambano, viboko hawa hawatakuwa na budi kuanza maisha na mtawala mpya.
Kasheshe ipo kwetu sie binadamu ambapo sometimes sababu za ma-ugomvi yetu zinakuwa hazieleweki na zikieleweka zinakuwa hazielezeki.

[Picha zote ni Ngorongoro crater, ahsante ya picha TTB]

No comments:

Post a Comment