Sunday, April 18, 2010

Mount Meru

Ni Mtiririko wa picha za Mlima Meru ambazo zimepigwa ktk angle tofauti tofauti ndani na nje kidogo ya manispaa ya Arusha. Juu ni Mtaa mmoja katikati ya Arusha (jina limeniteleza kidogo). hii ilikuwa ni May 2009.

Usa river, njiapanda ya kwenda Arusha national park. hii ilikuwa ni December 2009.

May 2009 mitaa ya kati Arusha.

Mwaka unajionyesha ktk picha, eneo ilipopigwa picha ni Kijenge flats. Ni raha iliyoje ukiwa unaamka asubuhi na kupata mandhari nzuri ya mlima Meru ukitokea ktk balcony yako! hii ilikuwa ni mida ya alfajiri.

Ndani ya Arusha national park karibu na Ziwa Mommella kubwa. December 2009.

Tokea Arusha Airport. Hii ilikuwa mwaka 2008 wakati uwanja huu ulipokuwa ktk mchakato wa kupigwa sop-sop. Picha zote ni kutoka ktk maktaba ya TembeaTz Blog.

No comments:

Post a Comment