Wednesday, March 31, 2010

Udzungwa Mountains National Park

Udzungwa Mountains National park sio hifadhi maarufu kwa wengi kama zilivyo Serengeti, Manyara, Tarangire, Ngorongoro na nyinginezo. Kikubwa kinachofanya wengi tusiifahamu yawezekana kuwa ni kutokana na kutokuwepo kwa wanyama wengi ambao ndio huwa kivutio kikubwa kwa wazalendo wengi. Ukweli unabaki kuwa Udzungwa Mountain National park ni hifadhi ya kipekee ambayo ni mahususi kwa wale wanopenda kwenda kuona miti, Viumbe hai wadogo na wa kati ambao hustawi ktk misitu ya ki-tropiki. Hii hifadhi ipo mkoani Morogoro. Kufika huku unapita bwawa la Kidatu.

Hifadhi hii imetawaliwa na milima na misitu yenye miti mirefu inayofunika ardhi jambo ambalo ktk sehemu nyingine, mchana unageuzwa kuwa usiku. Safari ndani ya hii hifadhi ni kwa miguu, Magari unaachana nalo getini. Aina hii ya safari huitwa hiking. picha juu ndio moja ya 'Highway' zilizopo ndani ya Udzungwa Mountains NP.

Uwepo wa msitu unatoa uhakika wa maji kuwepo kipindi kirefu. Hali ya milima imepelekea Udzungwa kuwa na maporomoko mengi ya maji ambayo nayo ni kivutio tosha cha kipekee humu nchini.
Uduzngwa inasimamiwa na TANAPA (kwa kuwa ni national park) ndio wanaohusika na kulinda na kuhifadhi msitu huu na maliasili zote zilizomo ndani yake. Sehemu ambayo mto unakatiza, jamaa wamejenga madaraja yanayowezesha wageni kuweza kuvuka mito na kuendelea na safari zao bila bugudha.
njia ambazo wageni wanapita wanapokuwa wanafanya hiking huitwa trails kwa lugha ya wenyewe. picha juu ni moja ya njia ambazo mgeni hupita anapokuwa anatembea ndani ya hifadhi ya Udzungwa Mountains.

Sanje Waterfalls ndio waterfalls maarufu sana ndani ya Udzungwa NP. Umaarufu wake unakuja kutokana na kwamba ndio waterfalls ndefu zaidi - 180m. Sio sehemu ya kukosa kutembelea ukienda Udzungwa Mountains NP.

Unapokuwa umesimama juu inapoanzia sanje waterfalls unapata view mwanana ya mashamba ya Miwa ya Kilombero Sugar. Makazi unayoyaona kati (msitu) ni kijiji cha Mang'ula.

Inaelezwa ya kwamba ukiwa Uduzungwa Mountains NP unaweza pia kuona baadhi ya maeneo ya pori la akiba la Selous. Ahsante ya picha TTB.

No comments:

Post a Comment