Wednesday, March 31, 2010

Mandara Hut

haya ndio mabanda ambayo wapanda mlima hupumzikia wafikapo ktk kituo cha Mandara hut. Mandara ni point ya kwanza kubwa ktk marangu route baada ya kutoka marangu gate. yenyewe. Ni umbali wa karibu kilomita 8.5 toka Marangu gate. Mandara hut ipo Mita 2700 juu ya usawa wa bahari.
Mabanda madogo ni kwa ajili ya malazi. Kubwa la mwisho ndio mess kwa ajili ya misosi. Mpishi inabidi mje nae; vyote hivi ni ktk gharama unazolipia kwa ajili ya safari ya kupanda mlima.


Juhudi za kuongeza mabanda zaidi ili kwenda sambamba naongezeko la wageni unaendelea. Picha juu inaonyesha moja ya mabanda ambayo yapo ktk hatua za mwisho za ujenzi hapo Mandara hut.

Mandara Hut kuna mandhari murua na tulivu. Sehemu kubwa ya safari toka Marang gate hadi kufika mandara inakuwa ipo ktk Msitu mnene ambao ni sehemu ya Kilimanjaro national Park (KINAPA). oicha juu ni sehemu ya msitu huo unavyoonekana toka Mandara hut.

No comments:

Post a Comment