Monday, March 29, 2010

Lunch ndio hii mazee....

Unapokuwa unapanda mlima na muda wa lunch ukiwakuta mkiwa katikati ya safari, (sio ktk huts) mlo huwa kama unavyoonyoeshwa ktk picha juu. Endapo kama utakuwa na mahitaji tofauti kampuni inayoandaa safari yako inaweza kukuandalia kitu mbadala. Cha msingi ni kuwaambia mapema. Picha juu ni lunch box Mdau aliyopewa wakati akipanda mlima Kilimanjaro mwezi Desemba mwaka jana. Endapo muda wa mlo ukiwakuta mkiwa ktk Camps/Huts basi hapo utapata menu tofauti.

Mlo huu hautofautiani sana na mlo utakaokula ukiwa ktk full day game driver Porini. Ktk Full day game drive, mara nyingi wageni huwa hawarudi hotelini/campsite kula lunch. Mnakuwa na packed lunch ambayo mnatoka nayo hotelini au campsite asubuhi. Muda wa lunch ukifika mnatafuta mahali panapowavutia na kuanza kula. Inaweza ikawa ni ktk maeneo maalum kama picknick sites au sehemu yoyote ile. Uzuri wa kutumia picknick site ni kwamba hapo mgeni anaruhusiwa kushuka toka kwenye gari na kukaa nje ya gari. Ilhali mkisimama sehemu ambayo sio picknick site, itabidi chakula mlie ndani ya gari. Hii ya kushuka inatoa fursa ya kujinyoosha na kula chakula ktk meza na pia ktk mbuga nyingine, picnick sites zinakuwa na sehemu za Adam na Hawa. Kwa kawaida Hotelini mnarudi jioni baada ya mizunguko kukamilika.

Hoteli za Porini huwa hazina mambo ya Half Board, malazi yao ni Full Board basis (Milo yote kwao). Kusimamia utaratibu wote wa misosi na mpango mzima ni vyema ukamwachia guide/driver. yeye ndie atakae wasiliana na hotel na kuijulisha kuhusu msosi wa kuchukua ktk full day game drive. kama una special needs, mueleze mapema ili afanye mipango murua.

No comments:

Post a Comment