Tuesday, March 23, 2010

Kijiji cha Mabira, Wilaya ya Karagwe; Kagera

Taswira maridhawa toka katika kijiji cha Mabira, Wilaya ya Karagwe Mkoani Kagera. Kijiji hiki kipo mpakani mwa Tanzania pamoja na nchi jirani za Rwanda na Uganda.

Wakati wa lile sekeseke la Rwanda mwaka 1994, njia hii ilitumika na raia wa nchi hiyo waliokuwa wakikimbia machafuko na kuja TZ kunusuru maisha yao. Wengi waliishia ktk kambi zilizoanzishwa na UNHCR huko Karagwe.


Kuzungumzia Mkoa wa kagera bila ya kutaja Kahawa na Ndizi unakuwa haujautendea haki mkoa huu. Picha mbili juu ni kahawa pamoja na Ndizi.

Rangi ya Kijani unayoiona imetanda ktk mlima huo sio Mahindi bali ni Migomba. Ahsante ya Taswira kwa mdau JM.

Moja ya aina ya utalii ambao inaanza kuchukua kasi hapa nchini ni ule utalii unaojulikana kama Cultural tourism. Hii ni aina ya utalii ambayo mgeni hutembelea jamii na kujifunza mila na desturi za jamii inayoishi mahali hapo. Aina hii inatoa fursa kujua mambo mengi mengineyo kuhusu watu na mazingira yao na utaratibu wa maisha yao pia. Mila na desturi za jamii huwa ni kivutio na pia jambo la kujifunza kwa mgeni.

No comments:

Post a Comment