Sunday, March 28, 2010

Jitahidi usiwe kati yao....

Unapokuwa mbugani na kukutana na mama na mwana Tembo, jitahidi kukaa mbali nao kwani Tembo hulinda na kuchunga sana watoto wao. Watawatetea kwa gharama yoyote ile, ikiwemo kukuvamia na kukugalagaza wewe mgeni wao.
Endeapo gari yako itakaa kati ya tembo na mwana Tembo, na kumfanya mama Tembo kushindwa kumuona mwanae kwa namna moja au nyingine; Tembo mama huanza kupata hisia kuwa mwanae kaibiwa/kapotea na hivyo hutaharuki na kuanza kuchafua amani ktk juhudi za kumsaka mwanae ambae wewe umemzinga kwa gari lako. Asipoweza kumuona haraka jua cha moto utakiona, na hata akimuona hujenga hisia kuwa jaribio lako limeshindwa na hivyo atafanya lolote ili ahakikishe usalama na amani kwa mwanae.

Ushauri wa bure ni kwamba ukiona mama na mwana tembo wapo pande tofauti za barabara, jaribu kuwa na subra hadi watakapokuwa pamoja kama mdau Tom wa kimasafaris alivyofanya ktk picha juu alipokuwa Tarangire NP mwezi Desemba mwaka jana. Kuingia kati yao, si jambo jema kulifanya after all porini hakutaki parapara na haraka.

Tembo hubeba ujauzito kwa muda wa Miezi 20! Huweza kuwa ktk hali ya kupata ujauzito akifikisha umri wa miaka 13. Muda mrefu wa kulea ujauzito ndio unaompelekea Tembo jike kuwa mkali kwa yeyote anayetishia usalama wa mwanae.

No comments:

Post a Comment