Sunday, March 21, 2010

Japo ni Porini, barabara zinaridhisha

Kusini mwa Serengeti NP

Kaskazini mwa Serengeti NP

Ruaha

mi-10

Hifadhi ya Taifa ya Arusha National park

Ngorongoro Crater

Tarangire

Selous Game reserve

Barabara ndani ya vivutio vyetu hapa nchini zipo ktk hali ambayo inatia matumaini na kuleta hamu ya kwenda kuvitembelea. zipo baadhi ya sehemu korofi (kutokana na hali ya eneo) lakini kwa kiasi kikubwa barabara nyingi zipo ktk hali ya kupitika mwaka mzima. Hili ni jambo ambalo mamlaka zinazohusika na usimamizi zimejitahidi na kiuungwana zinastahili pongezi. picha juu ni baadhi tu ya barabara ktk mbuga na hifadhi mbalimbali za hapa nchini ambazo tembeaTz inakuletea kukupa hali halisi ya barabara zake.

Kwa kuhofia usalama wa wanyama, barabara nyingi zilizopo ndani ya haya maeneo hazijawekwa lami. Barabara pekee ambayo inakatiza ktk hifadhi na ina lami ni barabara kuu ya Iringa-Morogoro ambayo inapita mi-10 NP.

licha ya kwamba barabara zipo ktk hali ya kuridhisha, bado mgeni anashauriwa sana atumie gari ambayo ni 4x4 ili kuondoa nafasi ya kukwama kwa namna moja au nyingine. licha ya hili, gari ambayo ni 4x4 inamuweka mgeni ktk nafasi nzuri ya kuweza kuona vivutio vizuri kwani zipo juu ukilinganisha na gari ndogo - saloon.

2 comments:

  1. Asante kwa habari hii, naomba ufafanuzi kidogo katika lami na usalama wa wanyama sijakupata vizuri hapo.

    ReplyDelete
  2. barabara za mbugani hazipigwi lami, ili kuacha nature iendelee kushika hatamu,pia inapunguza gari kwenda speed isije hatarisha maisha ya wanyama.hata hivyo kuna sheria na fine kwa yeyote atakayemgonga mnyama mbugani,ili madereva wawe makini wawapo mbugani.

    ReplyDelete