Sunday, March 21, 2010

Bush Breakfast - Balloon safari; Serengeti

Balloons zikitua, kinachofuatia huwa ni kifungua kinywa ambacho abiria na crew ya balloon mnapewa chini ya mti, ndani ya hifadhi (Hakuna uzio wala nini, hapo ni ndani ya hifadhi kabisa). wenye lugha yao wanaiita hii kitu Bush-Breakfast. wanaondesha safari za hizi balloons wameruhusiwa kufanya hizi shughuli ktk sehemu kadhaa, hapo ni moja ya sehemu iliyotumika siku ambayo timu ya TembeaTz ilikuwepo. Mnaletwa hapa na magari ya kampuni ya Balloon Safaris.

Ni utamaduni ya kwamba kitu cha kwanza ni kufungua mvinyo (Champagne) ili kusherekea safari salama. Siku hiyo kuliruka mapulizo mawili, na hao wanaofungua mivinyo ndio waliokuwa marubani. Kulia ni Capt Mohamed ambaye ndie alirusha pulizo ambalo team ya TembeaTz ilipanda.

Mambo yote unayotegemea kuyapata ukiwa ktk restaurant kubwa unakutana nayo hapa. Sometimes inakuwa ngumu kuamini kuwa upo katikati ya Hifadhi ya Serengeti. Siku hii kulikuwa na abiria kutoka mataifa mbalimbali.

Baada ya Staftahi ya porini, maongezi ya hapa na pale hufuata.

Eneo la tukio kwa mbali kidogo; magari yanakuwa yameegeshwa barabarani (Kulia).

Kulia - kushoto kote kumezungukwa na nyasi na miti michache, hapa ni maeneo ya kati kati ya ndani ya hifadhi ya Serengeti.

Baunsa akiwa pembeni akiangalia wadau. Nyuma ya baunsa ni sehemu ya kunawia ukiwa unatoka maliwatoni (Tent la kijani nyuma zaidi ya baunsa, pembeni ya mti).

Mwisho wa siku baada ya kupata staftahi ya porini, kampuni ya balloon inakurudisha hapa; Seronera Wildlife lodge mahali ambao guide/dereve wako anatakiwa kuja kukuchukua ili muendelee na ratiba zenu nyingine. Hizi safari zina utaratibu ambao operators na guides wao wanaulewa vilivyo. Ni vyema sana ukawasiliana na tour operator wako wa karibu ili ausimamie mpango mzima. Ki ukweli, Balloon safaris ina msisimko mwanzo hadi mwisho wake, kumbukumbu zake utabaki nazo kipindi kirefu.

Picha juu ni sehemu ya mbele ya Seronera wildlife lodge, Hii ni moja ya hoteli kongwe sana ndani ya Serengeti.

2 comments:

  1. Najaribu kufiri, kama sharubu akitokea itakuaje.

    ReplyDelete
  2. sharubu akitokea ndio kati ya starehe zenyewe mdau.

    ReplyDelete