Ikiwa wewe ni mpenzi na mnazi wa mambo ya wanyama pori lakini unakosa muda wa kwenda porini kutembelea na kuwaona wanyama wakiwa ktk mazingira yao, Dar Es Salaam Zoo inakupa nafasi ya kuwaona wanyama wakiwa ktk Zoo hii. Dar Es Salaam Zoo ipo maeneo ya kibada, Kigamboni nje kidogo ya jiji letu. Ni Sehemu murua kutembelea na familia na kujionea wanyama na ndege mbalimbali. Timu ya TembeaTz iliwahi fanya ziara yake maeneo haya mwishoni mwa mwaka jana. Picha juu ni ndege aina ya Marabou Storks ambao na wapo DSM zoo. Wadau wanaoishi kando kando ya ziwa Victoria (maeneo yenye shughuli za uvuvi) wanawaelewa hawa ndege.
Wana collection ya ndege mbalimbali wa porini ambao wanawekwa ktk banda moja, hapo utawakuta Flamingo, Egyptian geese, aina mbalimbali ya Storks, Hornbills, Bata mzinga na kadhalika.
No comments:
Post a Comment