Thursday, February 18, 2010

Viingilio na taratibu za Serengeti NP

Ukiangalia ubao wa matangazo utajionea ni jinsi gani TANAPA inavyowawekea wazawa mteremko wa kuweza kuzitembelea hifadhi zetu na sehemu mbali mbali. Tofauti ni kubwa mno kati ya Mtanzania na yule asiye raia.
Baadhi ya taratibu muhimu za kuzingatia unapokuwa ndani ya hifadhi ya Serengeti. licha ya kwamb ubao huu upo Serengeti, lakini ki ukweli hizi taratibu zipo applicable ktk hifadhi za taifa zote.

licha ya kutoa punguzo la viingilio, kuna haja kubwa ya kuwa na nguvu za pamoja ili kuweza kuongeza idadi ya Watanzania wanaotembelea hifadhi mbali mbali zilizopo nchini. Swala hili lina marefu na mapana yake, TANAPA wamejitahidi kwa uwezo wao. Changamoto inabaki kwetu wadau wengine ili kutimiza azma ya Utalii wa ndani. Utalii wa ndani ukipanda, uwezekano wa kuondokana na msimu wa utalii (High na Low season) upo. mwaka mzima ukawa ni msimu wa utalii. Njia mojawapo ya kutimiza azma ya kupeleka watanzania wengi ktk hifadhi na mbuga zetu ni kwa kufanya safari za makundi ili kuweza kupunguza gharama mbali mbali za safari za porini. hili si jambo geni kwani hata 'watalii wenyewe' wengu huja kwa makundi ili kupunguza gharama kwa upande wao.

No comments:

Post a Comment