Monday, January 4, 2010

Momella Kubwa - Arusha national Park

Arusha national Park. Ukiingilia gate la Ngurdoto itakuchukuwa kama saa moja kuyafikia maziwa haya. ukiingilia gate la Momella, safari inakuwa ni fupi ziadi (chini ya nusu saa). yote kwa yote, endapo utatembelea Arusha national Park jitahidi walau ufike ziwa Momella ndogo ambalo linafikika kirahisi. Juu ni Ziwa Momella kubwa

ukikuta ziwa au bwawa limejaa hawa jamaa, basi ujue maji ya hilo ziwa au bwawa sio fresh. Flamingo hushamiri sana ktk maziwa ambayo maji yake ni alkaline. ktk mazingira hayo hupatikana brue-green algae ambao ni msosi kwa flamingo.
bofya hapa kwa dondoo zaidi kuhusu ndege hawa

Mandhari tulivu.
Dondoo muhimu kuhusu ziwa la Momella kubwa. kama simu yako inasoma network ya kidhungu basi utakutana na data kuhusu ziwa Rishateni: ni ziwa ambalo 'linasemekana' kuwa na concentration kubwa ya Flouride duniani. wataalam wa mambo haya tunaomba msaada kuhusu hili swala. nasikitishwa na uwepo wa neno 'Probably' ktk maelezo kwenye huo ubao.
Ni jukumu la nani kuhakikisha na kuthibitisha hili?

Mvua kubwa iliyonyesha muda mfupi baada ya kupiga picha hizi sambamba na muda wa kuendelea kubaki mbugani kuelekea ukingoni, kulisababisha squad ya TembeaTz kushindwa kulitembelea ziwa la Rishateni kwa karibu na kupata data zaidi za ziwa hilo.

1 comment:

  1. Nilipata kusikia kuwa, uwepo wa florides kwa wingi kwenye maji (mito na maziwa) Arusha ndiyo sababu ya Watu wa huko kuwa na meno yenye kutu. Inawezekana kabisa kuwa wingi wa hizi fourides umesambaa kwa kiasi kikubwa Arusha na maeneo yanayoizunguka. Kutu ya meno ni dalili ya ugonjwa uitwa Dental Fluorisis.

    ReplyDelete