Thursday, December 31, 2009

Arusha National Park - dakika 25 toka Arusha mjini

Ni mwendo wa takriban dakika 25 toka Arusha (ukielekea Moshi) USA River mbele kidogo unakata Kushoto - Njia ya kuelekea Ngurdoto mountain lodge unakutana na Arusha National Park (ANAPA). Ni hifadhi murua yenye mchanganyiko wa wanyama na mandhari tulivu ya milimani. ipo ktk maporomoko ya Mlima meru. ndani ya Mbuga hii ndio kuna moja ya route ya kwenda kuukwea mlima Meru. Ni pazuri na mojawapo ya mbuga ambazo zipo karibu sana na mji mkubwa (Arusha) na hata makazi ya watu. Hapa hakuna Simba, predator mkubwa hapa ni Fisi na Chui ambao wanaonekana kwa nadra sana maeneo ya Ngurdoto crater.

Ukipita lango kuu la kuingia hifadhini, unakutana sehemu inayoitwa Serengeti Ndogo. hapa hukosi kuwaona Nyati, Punda, ngiri, ndege kadhaa na wanyama wengine wanaokula nyasi waliopo ndani ya hifadhi ya Arusha.
Pundamilia na Ngiri wakiendelea kupata mlo ktk eneo lijulikanalo kama Serengati ndogo, ndani ya hifadhi ya Arusha.

Barabara ni nzuri na zenye kupitika muda wote. Timu ya TembeaTz ilikutana na baadhi ya wageni ambao walikuwa wanaitembelea mbuga hiyo kwa magari madogo (Cresta GX100) na yalikuwa yanaenda bila shida yoyote. kutokana na mbuga hiyo kuwepo ktk slopes za Mount Meru, vilima vya hapa na pale havikosekani.

Kuna sehemu utakutana na misitu ya miti inayoota maeneo ya milimani, kwenye baridi kali.

No comments:

Post a Comment