Ukiwa unapenda wanyama pori basi hata kama utaenda visiwani utatamani uwaone hata kama ni wadogo na wachache. Visiwa vya Zanzibar, vimejaaliwa kuwa na aina ya pekee ya mbega ambao wanapatokana Visiwani humo tu. Hao ni Zanzibar Red colobus monkeys - Mbega wekundu wa Zanzibar. Na msitu wa Jozani ndio eneo mahususi lililotengwa kuwahifadhi na kuwapa fursa wengine kuja kuwaona viumbe hawa adimu. Tofauti na misitu na hifadhi nyingi za Hapa nchini, Msitu wa Jozani mgeni hutembea kwa miguu kuwasaka Mbega walipo. inategemea na muda na hali ya mazingira kwani unaweza tembea kwa masaa kadhaa ili kuwapata. Siku hii ilituchukua muda mfupi sana kuwaona kwani ilikuwa ni mida ya jioni na walikuwa wamesogea karibu kabisa na geti la kuingilia kwenye hifadhi.
Tulilikuta kundi kubwa la mbega likiwa kwenye eneo lijulikanalo kama restaurant. Walikuwa ni kundi la mbega wapatao 30 hivi, wakubwa na wadogo - majike na madume. Tofauti na nyani, Mbega wao sio waoga wa binadamu na wanaweza kumsogelea mtu bila wasiwasi au wakakuruhusu ukawasogelea wao bila wao kuwa na shaka na wewe.
No comments:
Post a Comment