Sunday, October 6, 2013

Geti La Mtemere - Selous Game Reserve

Ni Moja ya mageti yanayoweza kukuingiza ndani ya Pori la akiba la Selous eneo ambalo limetengwa kwa utalii wa picha. Pori la Akiba la Selous limegawanywa katika maeneo mbalimbali kwa matumizi ya ki uhifadhi. Kuna maeneo yaliyotengwa kwa ajili ya Utalii wa picha na maeneo mengini ni kwa ajili ya shughuli za uwindaji wa kitalii pia. Utalii wa picha ni utalii ambao mgeni huingia porini kwa lengo la kujionea na kujifunza kuhusu wanyama pori na mazingira yao. ndio aina ya utalii ambo wengi wetu tumekuwa tukifanya kwenye maeneo tofauti tofsuti hapa nchini. Kwa Selous, mgeni wa utalii wa picha ataingilia aidha geti hili la Mtemere au geti jingine ambalo linajulikana kama Geti la Matambwe. Geti la Mtemere lipo Rufiji mkoa wa Pwani wakati la Matambwe lipo Kisaki, Morogoro. Kufika kwenye geti la Mtemere kwa njia ya gari (kutokea Dar) itamlazimu mgeni kupita Kibiti au Ikwiriri. Pembezoni ya geti hili kuna uwanja mdogo wa Ndege ambako ndege nyingi ndogo hufanya safari za kila siku kwenye uwanja huu. Uwanja huu mdogo wa ndege nao unajulikana pia kama Mtemere.

No comments:

Post a Comment