Wednesday, October 16, 2013

Daraja la Mto Wami - Saadani NP, Bagamoyo

Wami bridge, Saadani National Park, Bagamoyo
Pichani ni Daraja ambalo linaunganisha Mji wa Bagamoyo na hifadhi ya Taifa ya Saadani. Kukosekana kwa daraja hili miaka kadhaa iliyopita kulipelekea wageni wengi kulazimika kupita njia ya Mandera, baada ya Kuvuka Mto Wami kwa njia ya Chalinze - Segera. JWTZ walijenga Daraja hili ambalo linatumika sasa. Linapunguza mzunguko kwa kiasi kikubwa ukilinganisha na safari ya kupitia Kijiji cha Mandera. hii picha niliipiga tukiwa tunatoka Saadani Np kurudi Dar kwa kupitia Bagamoyo.

Wami bridge, Saadani National Park, Bagamoyo
Ni mwendo wa mmoja mmoja kama kwenye kuchukua majibu ANGAZA vile!

Wami bridge, Saadani National Park, Bagamoyo
Mwenzako akishalimaliza Daraja na wewe ndio zamu yako inaanza. Hakuna kupishana.

Wami bridge, Saadani National Park, Bagamoyo

Wami bridge, Saadani National Park, Bagamoyo
Kina cha maji siku hii kilikuwa chini kama kinavyoonekana tokea juu ya daraja.

Wami bridge, Saadani National Park, Bagamoyo

No comments:

Post a Comment