Friday, August 9, 2013

Vijimambo vya Mlimani

Kupanda Mlima Kilimanjaro sio jambo la lelemama, ni swala ambalo mpandaji anatakiwa awe amejiandaa kimwili na kiakili. Safari nzima ya kupanda (kwa njia ya Marangu) ni ya kilometa kama 70 za kutembea - endapo utafika kilele cha Uhuru. Hiyo ni kielelezo tosha cha urefu wa safari. Ukiachia na umbali huo, kuna swala la umbali toka juu ya usawa wa bahari - altitude. Ki ukweli, madhara ya hii ni ngumu kuyaelezea lakini kupanda mlima kwenye uwanda wa juu kunachosha sana kutokana na hewa kuwa na upungufu wa Oksijeni. Moja ya mambo ambayo mpandaji anaweza kuanza kuyasikia pale altitude inapoanza kimzingua ni kichwa kuuma, kichefuchefu na mwishowe kurudisha chenji kabisa, Tumbo kuvurugika na hata kupelekea mpandaji kuanza kuharisha na reaction nyingi nyinginezo. Hii huwatokea wengi wanapoingia umbali wa Mita 4000 juu ya bahari na kuendelea. kwa madhara mengi ya awali ya altitude sickness dawa ya kwanza ni kuanza kumshusha mpandaji kurudi kwenye uwanda wa chini ambako kuna hewa yenye oxygen ya kutosha. kama hali haitaboreka basi hufikishwa hospitalini ambako anapewa matibabu stahiki na kurejea kwenye hali ya kawaida. kwa walio wengi, kitendo cha kushushwa chini huwa ni tiba ya kumpa ahueni mpandaji na kumrudisha kwenye hali yake ya kawaida baada ya muda mfupi. 
Endapo Mpandaji atazidiwa kiasa cha kushindwa kujimudu mwenyewe, basi itawalazimu wasindikizaji wake wamshushe chini kwa kutumia machela ambazo ni maalum kwa matumizi ya safari za huku mlimani. Picha mbili za juu ni mgeni ambaye tulikuta akishushwa kuelekea kituo cha Horombo na 'wagumu' wake kilometa kadha kabla ya kufika kituo cha Kibo. Alianza Summit ascent usiku lakini akazidiwa akiwa njiani. Alishushwa na kurudishwa Kibo kwa mategemeo ya kuwa angepata ahueni lakini hali yake haikutengemaa kama ilivyotegemewa. uamuzi wa kumshusha chini zaidi ulifikiwa na hapo akiwa njiani kutoka Kibo kuelekea Horombo. Sisi tulikuwa tunaelekea Kibo tukitokea horombo. Wakati tukirudi tulipofika Horombo niliuliza habari za huyu mgeni na kuambiwa alifika Horombo akiwa anatembea mwenyewe licha ya kuondoka Kibo akiwa kwenye machela. Alipata nguvu baada ya kushuka chini. ndio Vijimambo vya Mlima Kilimanjaro

Hizi ni baadhi ya machela tulizozikuta kwenye parking yake ktk kituo cha Horombo. Huwa zinatumika zaidi kwenye hili eneo kati ya Horombo na Kibo. Hapo mgeni hufunikwa na mablanketi na kulazwa hapo juu ya machela na wagumu wawili au zaidi wanaiburuza hiyo machela kwa tairi lake. Mazoezi na kufuata maelekezo ya guides wako ni moja ya nguzo muhimu zitakazo kuwezesha kuupanda Mlima Kilimanjaro Salama salmin.

2 comments:

  1. Kama MTU ana afya ya mgogoro na hajiwezi kwa nini kuparamia mlima. Watalii wawe wanapima afya Zhao kabra ya kuanza safari.

    ReplyDelete