Sunday, May 5, 2013

"Kunguru" wa Mwanza

Mwanza
Ni ndege wanaoitwa Marabou Stork (mtanisamehe jina lao la Kiswahili silifahamu) ambao kwenye jiji la Mwanza naweza kusema ndio kama Kunguru wao. Palipo na soko la Samaki hawa ndege hawakosekani. Hawaogopi watu, wanajichanganya na watu bila wasiwasi. Kama wewe sio mwenyeji wa jiji la Mwanza (kama ilivyokuwa kwangu) unaweza ukaanza kuwaogopa wewe. Hapa ilikuwa ni kwenye soko dogo la Samaki liliopo pembeni ya chuo cha wanyama pori cha Pasiansi.

Mwanza
Unaweza ukaona si sawa wao kuwepo karibu hivi lakini kwa muda mfupi niliokaa sokoni hapa naweza kutoa uthibitisho wa kuwa hawa ndege ni muhimu kimazingira. licha ya kwamba hili ni soko la samaki lakini hapa utatafuta pezi au matumbo ya samaki na hutapata kitu. Hawa ndege wanadaka matumbo na mapezi ya samaki hata kabla hayajafika chini na wanayala mazima-mazima. Kimsingi wazoa taka wa jiji la mwanza sidhani kama wanahangaika na mabaki ya Samaki wanaovuliwa ziwa Victoria.

Mwanza Hawa wakiwa juu kwenye paa la moja ya majengo ya soko la samaki la Mwaloni.

Mwanza
Karibu kila kona ya soko la Mwaloni hawa ndege wapo wakisubiria mabaki ya samaki yanayotolewa wakati wa kuwasafisha. Picha hizi zilipigwa na kamera ya blog ya TembeaTz ndani ya jiji la Mwanza wakati wa weekend ya Pasaka 2013.

No comments:

Post a Comment