Hizi picha nilitumia mapema leo na Mdau Thomas wa HSK Safaris aliyeopo huko hifadhi ya taifa ya Serengeti. Picha ya juu imepigwa pembezoni mwa ziwa la Masek, Ziwa ambalo nalo lipo kusini magharibi mwa hifadhi ya Serengeti. Kwa mbali unaweza kuwaona nyumbu wanaohama wakilisogelea ziwa ili kuweza kukata kiu yao baada ya safari ndefu ya kukatiza mbuga ya Serengeti wakitokea Masai Mara. Maeneo haya ndio kama huwa ni mwisho wa Migration ambapo nyumbu hawa wanatarajiwa kukaa hapa huku kazi kubwa itakayokua ikiendelea ni kuazaa watoto kabla zoezi la kuhama halijaanza mzunguko mwingine.
Sharubu hawa nao hawakuwa mbali na shughuli nzima ya wahamaji. Nao walikuwa pembezoni ya ziwa Masek ili nao waweze kujipanga na kuambulia chochote kitachoingia kwenye 18 zao.
Picha zote toka kwa Mdau Thomas wa HSK Safaris
No comments:
Post a Comment