Tuesday, February 12, 2013

Maboresho ya Crater View Point - Ngorongoro

Ngorongoro Crater
Ni Ile sehemu ambayo wageni wanaoingia eneo la hifadhi la Ngorongoro hupata fursa ya kwanza kujionea ukubwa na maajabu ya Ngorongoro crater kwa juu wakiwa njiani kuelekea kwenye geti la kushukia crater. Eneo hili hujulikana kama Crater view point na kwa muda mrefu pamekuwa ni eneo la wazi. Wasimamizi wa Ngorongoro crater wameanza kupafanyia maboresho kama ambavyo Mdau Aenea wa Tanzania Giraffe Safaris alivyonasa taswira hii ambapo uzio umewekwa.

No comments:

Post a Comment