Ndinga ya Lakeland Africa ikiwa ndani ya kivuko cha MV Pangani sambamba na watalii wake.
Hapa wakiwa kwenye lango la kuingia kwenye ofisi ya mkuu wa wiliya. Jengo hili ni moja ya majengo ya kihistoria kwani lilitumika na wakoloni pia. Picha wanayoonyeshwa ni ya Rais Jakaya Kikwete ambapo baba yake mzazi alikuwa ni mkuu wa wiliaya wa kwanza wa Pangani baada ya Tanganyika kupata Uhuru wake.
Watalii wazalendo wakikatisha mitaa mbalimbali ya mji wa Pangani
Nyumba aliyokuwa akiitumia Abushiri kujificha dhidi ya Wajerumani ikionekana juu ya Kilima pembezoni ya mto Pangani. Picha hii imepigwa tokea kwenye boti. maji unayoyaona ni ya mto Pangani.
Walipiga Kambi YMCA Pangani.
Machweo pembezoni ya mto Pangani. Picha zote zimetoka kwenye ukurasa wa Facebook wa Lakeland Africa ambako kuna picha zaidi ya hizi. Ungana nao ili uweze kupata picha na kujua matukio yanvyoendelea kwenye safari hii ya sasa. Kumbuka Safari nyingine kama hii itaanza rasmi mwezi January 2013 kama ilivyotangazwa awali.
Bofya hapa kupata dondoo za Mji wa Pangani toka Wikipedia
No comments:
Post a Comment