Monday, December 31, 2012

Majiko ya Camping

Wildness Safaris Tanzania - Camping Selous Game Reserve
 Ni nyenzo kadhaa ambazo zimekuwa zikitumika kuanda misosi kwa wageni wanaofanya tented camping huko maporini. Picha hizi zilipigwa siku nyingi kidogo kipindi ambacho matumizi ya nishati ya gesi hayajashika kasi. Sasa hivi asilimia kubwa ya mapishi ya camping hutumia nishati ya gesi asilia inayobebwa kwenye mitungi.

Wildness Safaris Tanzania - Camping Selous Game Reserve
 Unaweza ukawa unajiuliza ni kitu gani ambacho kimekalishwa kwenye moto/mafiga, Hilo ni moja ya yale masanduku ya bati ambayo kwa rafiki zangu mliosoma shule za boarding mtakuwa mnayafahamu fika. Kipindi hicho yalikuwa yakiitwa Mizinga, sijui kizazi cha sasa kimeyapa jina lipi. Huu mzinga una kazi nyingi ikiwemo kutumika kama oven ya kuokea mikate au kukamilisha mchakato wa kuivisha wali aka ubwabwa.

Wildness Safaris Tanzania - Camping Selous Game Reserve
Mapishi yakiwa yanaendelea. mzinga unaweza kutumika kuokea mikate na hata cake ikibidi. Hali ambayo inamfanya mgeni asipate tofauti ktk maakuli yake na kumfanya asitambue kuwa amefanya tented camping safari. Ni ubunifu ambao unahakikisha mgeni anapata kile roho yake inapenda popote alipo na kwa kadri mazingira yanavyoruhusu

Wildness Safaris Tanzania - Camping Selous Game Reserve
Picha zote zimepigwa ndani ya pori la akiba la Selous na Mdau Rajab wa Wildness Safaris Tanzania

2 comments:

  1. Nimependa idea ya mzinga...sasa kufuli la nini si wote mpo wamoja hapo ...hahahaa

    Mjombaa!!!....

    JM

    ReplyDelete
  2. hahahaaa limetoka kiwandani kwetu ilo...

    ReplyDelete