Wakati wa Uzinduzi wa Karibu fair Mwaka jana huko Arusha, Aliyekuwa Naibu waziri wa viwanda na Biashara Mhe. Lazaro Nyalandu alidokeza kuhusu Tanzania kama nchi kuwa ktk uhaba wa huduma za Hoteli za kiwango cha juu. Hali ambayo inainyima nchi fursa ya kuandaa na kuhodhi Mikutano na makongamano makubwa ya kimataifa. Uhaba huu upo mijini na hata kwenye maeneo yenye vivutio mbalimbali vya utalii.
Blog ya TembeTz imepokea habari za kusogezwa mbele kwa Tamasha la Karibu Fair huko Mkoani Arusha mwanzoni mwa mwezi ujao. Awali tamasha hili lilikuwa lianze Tarehe 1 mpaka 3 Juni 2012 lakini habari ambazo Blog yenu imezipata ni kwamba Tamasha la Karibu limepelekwa mbele kwa wiki moja ambapo litakuwa tarehe 8 mpaka 10 Juni 2012. Blog yenu imedokezwa ya kuwa uwepo wa mkutano mkubwa wa sekta ya benki mkoani Arusha unaowaleta wadau wa sekta ya benki toka Duniani kote kuwa ni chanzo cha mabadiliko ya tarehe ya Karibu fair. kikubwa ikiwa ni uhaba wa huduma za malazi kwa wageni wa shughuli hizi mbili kama zingeachwa kuendelea kwa wakati mmoja. Shughuli zote mbili zinaleta mamia ya wageni na washiriki toka nje ya mkoa wa Arusha na Nje ya nchi kwa ujumla. Wote hawa wangehitaji mahali pa kulala jua linapozama jambo ambalo mkoa wa Arusha umeonekana kutokuwa na uwezo wa kukidhi mahitaji ya wageni hawa.
Pindi tutakapopata tamko rasmi kuhusu mabadiliko haya tutayaweka hewani japo tayari tovuti ya Karibu Fair imeshafanyiwa marekebisho na kuanza kuonyesha tarehe mpya za tamasha hilo. Hivi Sasa Mhe. Nyalandu ni naibu waziri ktk wizara ya Maliasili na Utalii baada ya mabadiliko ya baraza la mawaziri yaliyofanywa hivi karibuni na Mheshimiwa raisi wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Kikwete. Ktk uzinduzi wa karibu fair mwaka jana, Mhe. Nyalandu alikuwa anamuwakilisha Waziri Mkuu ktk uzinduzi huo. Video hii ni ya mwaka jana lakini ukweli wa yalisemwa umejithihirisha sasa hivi huko mkoani Arusha.
unaweza kujionea video zaidi ktk youtube channel ya tembeatz kupitia
No comments:
Post a Comment