Tuesday, May 29, 2012

Maandalizi ya Karibu Fair (Arusha) 2012 yanaendelea vizuri


 Maandalizi ya eneo ambapo Maonesho ya KAribu Travel & Tourism 2012 yatafanyika yanaendelea vyema bila chenga licha ya mabadiliko ya tarehe yaliyojitokeza. Maonesho haya hufanyika kila mwaka kwenye uwanja wa Magereza, nje kidogo ya jiji la Arusha - Karibu na Arusha airport. Kila mwaka maonesho haya hufanyika weekend ya kwanza ya mwezi Juni japo mwaka huu yatafanyika kuanzia tarehe 8 mpaka 10 Juni ili kupisha mkutano mkubwa wa kimataifa wa sekta ya Benki unaofanyika Mjini Arusha. Mtundiko huu unakuletea taswira kadha wa kadha za maandalizi ambayo yanaendelea kuhakikisha kuwa maonesho yanaendelea bila dosari.

 Mvua zilizotangulia zimeufanya uwanja huu kuwa na majani ya kutosha mwanzo mwisho.

Mahema kwa ajili ya kuwahifadhi washirikia yakiendelea kusimikwa.

Hema la Kijani kushoto ni Ofisi ndogo ya Team ya Karibu fair inayoratibu shughuli mbalimbali za maandalizi hapo uwanjani hivi sasa.

 Moja ya ndinga zinazotumiwa na waratibu wa maandalizi likiwa limeegeshwa kivulini.

malighafi zaidi za ujenzi zikiletwa eneo la kazi ili kazi isonge kama iivyopangwa

Hema la kupatia maakuli na mapumziko kwa huduma mbalimbali kwa wafanyakazi wanaoendelea na shughuli za maandalizi uwanjani.

Makampuni na wadau wa Utalii wanahimizwa kushiriki kwenye maonyesho haya ambayo hufanyika kila mwaka hapa nchi yakiwaleta wadau toka kila kona ya Dunia kuonyesha kazi na shughuli zao kwenye sekta ya Utalii. Ni Maonesho ya siku tatu ambayo hutoa fursa ya wadau kubadilishana mawazo na hata kufungua fursa mpya za biashara baina ya makampuni mbalimbali. Karibu Fair imekuwa ndio kama saba-saba ya sekta ya utalii kwa hapa nyumbani na katika ukanda huu wa Africa Mashariki. Hakuna maonyesho mengine makubwa na yenye kuheshimika kama Karibu Fair.

Akizungumza tokea Arusha kwa njia ya simu, Mdau Sam Diah ambaye ni mmoja wa waratibu wa maonesho haya amesema makampuni mengi yameshathibitisha ushiriki wao licha ya mabadiliko ya tarehe za maonesho. "takriban asilimia 95 ya washiriki wameshathibitisha ushiriki wao kwenye tarehe mpya. Haya ni makampuni ambayo yalishathibisha ushiriki wao kwa zile tarehe za awali". "haya asilimia 5 bado yanaangalia ratiba yake kabla ya kufanya uamuzi, matarajio yetu ni kwamb nayo yatashiriki pia". Aidha, Sam ameidokeza TembeaTz kuwa tayari makampuni mengi ambayo yanashiriki yameshaanza kuwaalika wadau kutembelea mabanda yao kipindi cha maonesho haya. "Email za 'See you at Karibu fair 2012' au kuomba appointments kwenye Karibu Fair zimeshaanza kuzunguka kwa wadau kuwakaribisha wadau wenzao kwenye mabanda yao" aliongeza Sam.
Kwa makampuni au wadau binafsi ambao wangependa kushiriki nafasi bado zipo wazi na hivyo kwa yoyote ambae anataka kuwa na banda afanye mawasiliano na Karibu Fair: info@karibufair.com  (Bofya hapa kwa details zaidi). Kwa wale waliopo Arusha wanaweza kufika Ofisi za Karibu Fair ziliziopo Corridor Spring hotel, Nyuma ya Kibo Palace Hotel kwa taarifa zaidi.
Endelea kuwa sambamba na Blog ya TembeaTz kwa taarifa na dondoo mbaliambali za maandalizi ya Maonesho haya kwa mwaka huu. Hii itakuwa ni mara ya pili kwa TembeaTz blog kushirikiana na wadau wa Karibu Fair bega kwa bega kukuhabarisha kuhusu maandalizi na mpaka maonesho yenyewe. 
Picha zote kwa hisani ya Mdau Sam Diah - http://www.karibufair.com/

No comments:

Post a Comment