Mdau Tom wa kima safaris alimfumu sharubu huyu dume akila pozi pembeni ya kundi la masikio lilikuwa linapumzika ktk hifadhi ya taifa ya Mikumi. Licha ya kwamba alionekana kuwa kama anapumzika, sharubu huyu alikuwa akila chaba kama kuna chochote anaweza kupata na kulinda ustawi wake toka ktk kundi hilo la masikio.
Unaweza kudhani mpambano kati ya sharubu na masikio ni kitu cha kusadikika, ukweli ni kwamba wanapokuwa ktk kundi sharubu wanauwezo wa kumwangusha masikio hususan wadogo au wale saizi ya kati. Ni dhahiri kabisa sharubu huyu ktk mtundiko huu alikuwa anali fanyia tathmini kundi la masikio hao. picha na mdau Tom wa Kima Safaris
No comments:
Post a Comment