
Utaratibu huu umewekwa ili kuondoa ulazima wa kuwa na sehemu za kutupia na kuharibu taka ngumu ndani ya hifadhi. nilidokezwa ya kwamba awali wapandaji walikuwa wakitupa taka ktk vituo vya kupumzikia na hapo zilikuwa zikikusanywa na kutupwa pamoja. utaratibu huu ulikuja kugundulika baadae ulikuwa unakaribisha wanyama hatarishi katika maeneo taka hizo zilipokuwa zinatupwa.
Usafi ni jambo ambalo linasimamiwa kikamilifu ktk route zito kuelekea uhuru point. jitahidi kadri uwezavyo kuonyesha ushirikiano kikamilifu nje ya hapo utalimwa fine na wahifadhi.
Picha juu ni baadhi ya taka ngumu nilizozilisha siku nilipofanya day trip. nilishuka nazo na kuja kuzitupa marangu gate wakati wa kutoka
No comments:
Post a Comment