Friday, December 10, 2010

Harufu ya pombe kali humkera......

Imekuwa ni jambo la kawaida kumwagia mafuta ya taa kwa lengo la kumfukuza ndani ya nyumba au kumuua kabisa nyoka anayeingia ndani ya nyumba au sehemu waliopo wanadamu. Ki ukweli kinachomkera nyoka ktk mafuta ya taa ni ile harufu kali ya mafuta ya taa. Harufu ambayo humchanganya akili na kumlevya hali ambayo hurahisisha kazi ya mvamiwaji (binadamu) kumuangamizi mvamizi wake. Wengi wameitumia njia hii kwa kupambana na nyoka wadogo wadogo au hata wale wa saizi ya kati pindi wanapokutana nao.
Kwa taarifa yako, hata chatu harufu ya mafuta ya taa humkera na uwepo wake unaweza kumfanya akaacha kuendelea na shambulizi lake na kutafuta njia ya kukimbia. Chatu nae ni nyoka hivyo kinachomkera nyoka mdogo, pia kina madhara yake (kikitumiwa vyema) kwa chatu pia.

Kwa wale waliosoma shule ya Sekondari ya Kibaha watakumbuka uwepo wa Chatu waliofugwa shuleni hapo kwa lengo la mafunzo. Niliwahi dokezwa ya kwamba chatu hao walikufa baada ya jamaa mmoja kupewa tenda ya kunyunyizia dawa ya kuulia wadudu ktk eneo karibu na banda lao. Bila ya kutambua madhara ya harufu ya dawa ile, chatu wale walikufa kutokana na harufu hiyo. Mfano huu unaongeza idadi ya nyenzo ambazo zinaweza tumika kupambana na uvamizi wa nyoka. Niliwahi pia sikia ktk documentary moja ya wanyama ambapo wao walienda mbali na kusema ya kwamba hata harufu ya pombe kali nayo ni mwiba mkali kwa nyoka tena hata chatu. ktk documentray hiyo (Untammed & uncutt) walikuwa wanaonyesha jinsi jamaa alivyong'atwa na chatu wake mwenyewe mguuni. Watu 3 walijaribu kubandua meno ya chatu yule lakini walishindwa mpaka pale chatu mwenyewe alipoamua kuachia. Mtaalamu wa nyoka alipokuwa akihojiwa kutoa tathimini ya nini kifanyike ktk situation kama hiyo, alieleza bayana ya kwamba hata pombe kali ingeweza kumkera chatu na kumfanya amwachie aliyemuuma. Chatu ana nguvu nyingi kukushinda. Kwa kutumia mabavu kamwe huwezi kumshinda. Kwa yule ambae mambo fulani (Pombe kali) yapo ndani ya nyumba, usisite kuyatumia endapo kamba (jina la nyoka porini) atakapokutembelea bila taarifa.

Picha zote zimepigwa Meserani snake park, Arusha ktk vipindi tofauti.

2 comments:

  1. Hii ni khabari mpya kabisa kwangu. Shukran kwa elimu hii!

    ReplyDelete
  2. KK ulipotea kwa muda kidogo lakini kama waswahili wasemavyo, kimya kingi kina mshindo. Leo nimerudi hapa na kukuta post iliyoniacha mdomo wazi. Sikuwahi kudhania kuwa Konyagi inaweza ikafukuza chatu. nitahikikisha maskani sikosi walau chupa 2 za konyagi. Moja ya kwangu nyingine silaha dhidi ya nyoka maana hizi mvua zilivyoanza hawakawii kuanza kukimbilia ndani.

    @Kimara

    ReplyDelete