Wednesday, October 27, 2010

Ukame umeshika hatamu....

Kuchelewa kwa mvua kumepelekea sehemu nyingi hapa nchini na hata nchi jirani kuingia ktk kipindi cha ukame. Licha ya kwamba dalili la za mvua zimeanza kuonekana, lakini tayari kuna baadhi ya maeneo yameathirika.

Licha ya kwamba kipindi cha kiangazi, hifadhi zetu huwa kame na kuzifanya zionekana kukosa mvuto. hali hii huwa na manufaa sana ktk kuweka sawa mfumo wa ikolojia ktk hifadhi. Kipindi hiki kinapofikia kiwango cha hatari, wanyama wanaokula nyasi hupata shida sana kutokana na nyasi kukauka au kutokuwepo kabisa. hali hii hupelekea baadhi yao kufa kwa wingi na kupunguza idadi yao. pia ukosefu wa maji ya kunywa huwa ni tishio la maisha yao. sambamba na sababu hizo, wanyama wanaokula wanyama wenzao wao huneemeka kwa kupata mawindo kirahisi. Kipindi cha kiangazi wanyama hulazimika kusogea panapopatikana maji ili kuweza kuyapata. Simba na wenzao hutambua upungufu wa vyanzo vya maji na hivyo hutega mitego yao ktk njia zinazoelekea yalipo maji au kuzengea pembezoni mwa mabwawa na mito inayokuwa na maji kipindi hicho. Hii huwahakikishia na kurahisisha upatikanaji wa mlo wao. Ki ukweli wala nyama huneemeka na ukame ilhali wala nyasi hutaabika na kuangamia.

mchezo hugeuka kipindi cha mvua au mara baada ya mvua kuisha. Nyasi na maji vinakuwa vinapatikana kwa wingi na ki urahisi. hali ambayo hupelekea mitego ya pembezoni mwa mabwawa kutozaa matunda. Kipindi hiki wala nyama huwa na wakati mgumu ktk mawindo kwani wala nyasi wanakuwa wanatapakaa sehemu nyingi na kufanya kazi ya kuwawinda na kuwaangusha kuwa nzito.

Hivi karibuni nilikuwa naangalia documentary ilikuwa inahusu matukio ya simba mla watu wa huko rufiji, takwimu za matukio ya simba kula watu kipindi hicho zilionyesha kuwa matukio mengi yalikuwa yanatokea kipindi cha mvua au mara baada ya mvua kukatika. Baadhi ya simba walikuwa wanashindwa kupambana ndani ya pori la akiba la Selous na hivyo kuamua kuingia vijijini na kushambulia raia wasio na hatia. Ni rahisi sana kwa simba kumshambulia na kumuua binadamu kushinda kumwinda nyumbu au hata swala. Hutumia nguvu kidogo kumshambulia binadamu. Ndio maana sharubu akila mtu ni lazima auwawe, hata acha na anaweza rudi tena ku-test zali.

Licha ya kwamba picha juu imepigwa Selous, hali ipo hivi ktk hifadhi nyingi za hapa nyumbani na hata zilizopo nchi jirani. mvua zikianza Novemba, hali itabadilika na Desemba green itakuwa kwa wingi. Picha juu imepigwa hivi karibuni na mdau Tom wa Kima Safaris ndani ya pori la akiba la Selous

No comments:

Post a Comment