Mdau Tom wa Kimasafaris alipata kulitembelea ziwa hili mwishoni mwa mwaka jana akiwa njiani kuelekea hifadhi ya taifa ya Katavi. Alisimama kwenye moja ya vijiji vinavyolizunguka ziwa hili na kutembelea maeneo kadhaa ikiwemo kufanya boat safari ndani ya ziwa hilo. Picha juu ni jamaa waliokuwa wanampeleka Tom na timu yake kwa ajili ya boat safari wakienda kuandaa mtumbwi wao tayari kwa safari hiyo.
Ziwa Rukwa ni moja ya maziwa ya hapa nchini ambayo yapo ktk eneo linalopita bonde la ufa. Mwinuko unaouona kwa mbali ni kingo za bonde la ufa.
Kuna baadhi ya maeneo pembezoni mwa ziwa hili yamezungukwa na matete na kutoa malisho kwa mifugo iliyo karibu na ziwa hili
KK, huyu samaki kwenye wavu huyu ni Kambale mdogo, si perege, perege umbo lake tafauti.
ReplyDeletesharubu hizo ni dalili ya catfish, yaani kambale kama alivyosema da Subi. lakini ni samaki anayeliwa, kwa ndugu zangu wa jangwani wasiojua kitoweo cha majini.
ReplyDelete