Thursday, September 30, 2010

bwawa la Mtera nalo limo ktk utalii

Wengi tunalihusisha bwawa la mtera na nishati ya umeme. Tena jina lake hutajwa sana nchi ikiingia ktk mzozo wa mgao wa nishati ya umeme. pasi na hayo, bwawa hili linavutia wageni kwa kuwapa fursa ya kupanda maboti yanayotumiwa na wanavijiji. Mdau Tom wa Kimasafaris hivi karibuni alilitembelea bwawa hili akiwa sambamba na wageni wake ambao walikuwa na shauku ya kuliona bwawa hili na kupanda maboti kama mtundiko huu unavyoonyesha. Safari huanzia kwenye mkokoteni unaosukumwa na punda. Hii ni muhimu kwani kina pembeni ya bwawa ni kifupi hivyo maboti hayawezi kufika mpaka pembezoni mwa bwawa na kuchukua abiria.

Wageni wakiwa ndani ya mkokoteni wa punda tayari kuelekea eneo lenye kina cha wastani ambako boti inakuwa inawasubiri.


Tayari kwa safari. boti hizi hutumika kwa shughuli za uvuvi ktk bwawa hili na pia kwa usafiri baina ya vijiji vilivyopo kando kando ya bwawa la mtera

Baada ya safari ya boti ndani ya bwawa, wageni hurudi na kushukia ktk mkokoteni kama ilivyokuwa awali na kurudishwa nchi kavu. Bwawa la mtera lipo ktk barabara inayounganisha mikoa ya Dodoma na Iringa. Bwawa hili lipo mpakani mwa mikoa hii

2 comments:

  1. Samahani, njia iliyo rahisi kufika Mtera toka Dar es Salaam ni kupitia Iringa au Dodoma?

    ReplyDelete
  2. Ingependeza zaidi kama ungetoa na maelezoppia namna ambovyo twaweza fika Mtera au hapo kwa kupanda mkokoteni

    ReplyDelete